RAPA muimbaji mahiri Bongo, anayemiliki Bendi ya Mapacha Orijino, Khalid Chuma maarufu Chokoraa hatimaye ameanza kujichanganya rasmi kwenye Muziki wa Gospo.

Kwa kipindi cha nyuma, mara nyingi bendi yake ilikuwa ikiimba nyimbo za Gospo lakini aliyekuwa akiimba nyimbo hizo ni mkewe, Catherine Chuma.

Kutokana na nyimbo hizo kuonekana kupendwa na bendi hiyo, Chokoraa naye ameo-nekana kuingia rasmi kwenye mpango wa kupiga nyimbo hizo ambazo juzikati akiwa na bendi hiyo katika Ukumbi wa Forty Forty uliopo Tabata Bima Dar naye alionekana kutumia muda mwingi kuimba nyimbo hizo.

Akizungumza na paparazi wetu Chokoraa alisema: “Mimi ni msanii kazi yangu ni kuwaburudisha mashabiki kwa staili yoyote nikitumia kipaji changu cha uimbaji.”