OBREY Chirwa mshambuliaji wa Azam FC ambaye jana aliiua Lipuli kwa kupachika bao la ushindi dakika ya 64 lililoipa Azam FC ubingwa wa kombe la Shirikisho (FA) amesema kuwa hana mpango wa kuondoka ndani ya kikosi hicho.

Kumekuwa na tetesi kwamba, Chirwa amegomea kuongeza mkataba ndani ya Azam na anahitaji kurejea Yanga jambo ambalo amesema si la kweli.

"Mimi ni mchezaji wa Azam FC bado nina mkataba nao hivyo sina mpango wa kuondoka kwa sasa," amesema.

Azam imetwaa ubingwa huo mara ya kwanza kwenye mchezo wa fainali uliochezwa uwanja wa Ilulu, Lindi.