RAPA wa kike anayetikisa kunako Muziki wa Hip Hop kutoka Marekani, Cardi B amekiri kupoteza mamilioni ya shoo kisa kufanya upasuaji wa mwili wake.

“Nachukia sana kukatisha shoo kwa sababu ya pesa. Naumwa kwa sababu ya pesa,” Cardi B aliweka kipande kifupi cha video chenye dakika 1:50 akiongea.

“Nalipwa pesa nyingi kufanya shoo. Ninakatisha shoo nyingi za mamilioni, lakini afya ni muhimu kwa hiyo nafanya vile naweza,” aliongeza Cardi B.

Hadi sasa, Cardi B ameshafanyiwa upasuaji wa matiti na hivi karibuni aliongeza upasuaji eneo la tumboni.