UGOMVI kati ya mwanamitindo maarufu wa Marekani na ambaye pia ni mwanamuziki, Blac Chyna na Familia ya Kardashian, haujakwisha, hii ni baada ya Blac Chyna kuionya familia hiyo kutotumia jina la mtoto wake Dream katika kipindi chao cha runginga cha Keeping Up With The Kardashians.



Chyna alipata mtoto huyo akiwa na mahusiano na Rob Kardashian, lakini baada ya kuachana amekuwa na mgogoro na familia ya Rob kwa madai kijana wao hatoi huduma kwa mtoto huyo.



Hata hivyo Kim, Khloe, Kylie wamekuwa wakimzungumzia mtoto huyo wa kaka yao kwa namna tofauti, lakini Blac Chyna alianza kumuonya Rob kuwa, aiambie familia yake iachane na mpango wa kumzungumzia mtoto wake.



Inasemekana kuwa Blac Chyna na yeye anataka kuwa na kipindi chake cha runinga ambacho kitakuwa kinajulikana kwa jina la The Real Blac Chyna, hivyo hayupo tayari kuona mtoto wake akizungumziwa kwenye vipindi vingine.



Vipindi vingine vinafanya vizuri kutokana na kutaja majina ya watu, Keeping Up With The Kardashians sitaki kuona wakimzungumzia mwanangu,” alisema Blac Chyna.