STAA wa Bongo Fleva, Bernard Paul ‘Ben Pol, amefunguka kuhusu mambo kadhaa yaliyoibuka kwenye mitandao  kutokana na baadhi ya watu kudai kuwa amemfuma mpenzi wake, Anerlisa ‘Anna’, akiwasiliana na mastaa wa muziki nchini Tanzania akiwemo Harmonize na Shetta,  jambo ambalo lilidaiwa  huenda wanamtongoza bidada huyo ambaye ni raia wa Kenya.Benpol anayetikisa na ngoma yake mpya ya WAPO aliyoiachia hivi karibuni baada ya ukimya wa muda mrefu, amesema hayo leo katika Kipindi cha Bongo 255 kinachoruka kila Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 10:00 jioni kupitia +255 Global Radio.

“Nakumbuka siku hiyo kuna kitu nilikuwa nafanya kwenye simu yake, ghafla ikaingia meseji DM ya Instagram, nikaingia nikawa naona majina ya mastaa wamemwandikia ujumbe, lakini nikaona hiki ninachokifanya sio kitu kizuri, hata kama ni mpenzi wako lazima umwachie privacy yake, huenda akawa anatafutwa kwa ajili ya biashara ama watu wengine wamemtumia proposal za kufanya naye kazi mbalimbali kwa sababu ni mjasiriamali.


“Kuandikiwa ujumbe na akina Harmonize wala haikunishtua kwa sababu ninamfahamu tabia zake, amekuwa akiandaa events mbalimbali na wao huwa wanakwenda sana kule (Kenya) kufanya shows kwa hiyo sikuona kama ni jambo la ajabu sana. Kuandikiwa ni jambo moja lakini ku-entertain ni jambo jingine.

“Hata mimi nilishawahi kupata kazi nyingi tu kupitia DM, sababu kupata namba mfano ya mkurugenzi wa kampuni flani inakuwaga ngumu sana, lakin DM ni rahisi kumpata mtu na ukawasiliana naye moja kwa moja, kwa hiyo niliona hilo jambo ni la kawaida sana wala watu wasifikiri labda Benpol alichukia, hapana. Watu wasione DM ni sehemu mbaya, hii ni sehemu nzuri kwa sababu inakuunganisha na watu tofauti.

Benpol livyokutana na mpenzi wake

“Mimi huwa nakwenda Kenya mara kwa mara, nilikwenda huko kwenye event moja, aliyenisaidia kuandaa event hiyo ni rafiki yake na Anna, baada ya event tukawepo tu tunapiga stori, akaniambia shughuli yake ‘nipo tu nauza maji’, sikutaka kuingia deep sana kuhusu kazi yake, tulibadilishana contacts, tukawa tunawasiliana, ninakwenda kule, tunatoka kidogo, tukapanga kufanya club tour, mimi nitangaze muziki wangu na yeye akawa anafanya activation ya maji yake, na baadae akaja Tanzania.