JESHI la polisi mkoani Pwani,linamshikilia Suleiman Issa Ngorombwe (43) mfanyabiashara na mkazi wa Mailmoja Tangini ,Kibaha,kwa kudaiwa kumbaka na kumlawiti binti yake wa miaka 11.

Kamanda wa polisi mkoani Pwani,Wankyo Nyigesa alieleza kwamba,tuhuma ziliripotiwa katika kituo cha polisi Kibaha Mjini Juni 20 majira ya asubuhi ambapo walimkamata mtuhumiwa.

"Baada ya upelelezi wa tuhuma hii kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani "

Alieleza,jeshi la polisi linaendelea kukemea vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na vya kinyama vinavyofanywa na baadhi ya watu kwenye jamii.

Wankyo alisema,vitendo vya aina hiyo huanzia ngazi ya familia hivyo alitoa rai kwa wananchi kutoa ushirikiano wa kuripoti taarifa za matukio kama hayo ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria na iwe fundisho kwa wengine.