Baada ya Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania kutangaza fununu za uwezekano wa shambulio la kigaidi kwenye Jiji la Dar es salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda usiku wa saa nane amelazimika kutoa taarifa hii kwa Wakazi wa Mkoa huo.
“Ndugu Wananchi wa Jiji la Dar es salaam, nimelazimika kuja kwenu usiku huu baada ya kupitia taarifa kadha wa kadha kwenye mitandao za kuonyesha tishio katika baadhi ya maeneo ya Dar es salaam na kuleta taharuki, ukweli ni kwamba Jiji letu lipo shwari, Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinafanya kazi kama kawaida”
“Niwatoe hofu walioko kwenye Mahoteli kwamba hakuna tishio lolote lile, ni vyema watoa taarifa wakazingatia Katiba ya Nchi yetu kwani tunavyo Vyombo maalum vya kutangaza kama kuna hali ya hatari” – Paul Makonda