MABINGWA watetezi wa kombe la Kagame, Azam FC kwa sasa wapo likizo kwa muda baada ya kutwaa kombe la Shirikisho FA na kumaliza ligi wakiwa nafasi ya tatu kwa msimu wa 2018/19.

Mratibu wa Azam FC amesema kuwa kwa sasa kikosi kinatarajiwa kurejea kambini Juni 20 mwaka huu kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mwaka 2019/20.

Pia wana kibarua cha kutetea kombe lao la Kagame huku michuano ikitarajiwa kuanza Julai 6 mwaka huu Kigali