Julius Somoire (26) kutoka nchini Kenya amenusurika kifo baada ya kuvamiwa na kung'atwa na fisi sehemu zake za siri ambapo ameitaka serikali kumfidia kufuatia majeraha mabaya aliyoyapata.

Mbali na kumjeruhi sehemu zake za siri, fisi huyo pia alimng'ata kwenye mikono na miguu pindi alipojaribu kuwaokoa mifugo wake aliokuwa akiwachunga eneo la Isinya Jumamosi, Juni 22, 2019.

 "Fisi huyo aliniuma sehemu zangu za siri, aliniumiza sana na sijui iwapo nitarejelea hali yangu ya kawaida, pia aliniuma kwenye miguu na mikono na kuniacha na majeraha mabaya", amesema Somoire.

Shirika la Wanyama Pori nchini humo (KWS) kutokana na shambulizi hilo limetakiwa kutafuta suluhu ya haraka ya kuwazuia wanyama pori kuvamia makazi ya watu.