MWANAMAMA Zarinah Hassan ‘Zari’ baada ya kutua nchini na kuhojiwa na mwandishi wetu alikiri kuvaa nguo zinazoitwa feki huku akiweka wazi kwamba anachoangalia yeye ni kupendeza tu. Zari alieleza hayo alipoulizwa kwamba anavaa nguo za gharama za kiasi gani ambapo alisema yeye huwa anavaa nguo yoyote, haijalishi

ni ya gharama kiasi gani isipokuwa iwe inampendeza. “Unajua mimi siwezi kukuambia kuwa ninavaa nguo za gharama flani ya juu, hapana, hata nguo za Kariakoo mimi navaa tu ili mradi ikikaa kwenye mwili wangu inanipendeza, si nguo tu hata nywele mimi navaa yoyote ile ili mradi nipo smati,” alisema Zari ambaye alionekana kuwajibu watu waliokuwa wakidai kuwa anavaa nguo feki za Kichina ambazo zimejaa Kariakoo