Kufuatia kuibuka kwa sintofahamu juu ya usajili wa mshambuliaji wa Yanga SC, Heritie Makambo kusajiliwa kwenye klabu ya Horoya ya nchini Guinea hali iliyosababisha Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera kuhusishwa na dili hilo.Mwenyewe Mwinyi Zahera amefunguka sakata zima la usajili wa Makambo huku akisema kuwa kamwe hausiki katika kumsimamia mchezaji huyo kama wakala badala yake aliombwa msaada ili kuepuka kutapeliwa kwenye vipengele vya mkataba.

”Waandishi wanaandika habari za uongo, na ukweli siwezi kusimulia mpaka pale mambo yakishakamilika, wamewahi kuandika Zahera anakwenda Ulaya kitu ambacho si cha kweli mapka msikie sauti ya Zahera mwenyewe au Makambo,” amesema Zahera.

Mwinyi Zahera ameongeza kuwa ”Mambo yapo kwenye mazungumzo na timu ya Horoya kweli, lakini mpaka mazungumzo yatakapo malizika ndiyo nitaeleza.”

”Safari yangu na Makambo nchini Guinea ni kuangalia namna gani mambo yatakavyokuwa, kusafiri sio kweli kuwa ndiyo kilakitu kimekamilika. Siwezi kuwaambia kilakitu ila mazungumzo bado yanaendelea, yatakapo malizika ndiyo nitawaambia.”

”Makambo bado ni mchezaji wa Yanga na ataendelea kuitumikia mpaka pale ligi itakapo kamilika, ataondoka na watu wote wata, Makambo sio mshambuliaji peke yake duniani ataondoka na tutapata wengine wazuri.”

Hata hivyo Zahera amefunguka kuwa kama dili la Makambo likifanikiwa kiasi chote cha fedha kitakachopatikana kitakwenda ndani ya Yanga SC.

”Makambo akinunuliwa na timu yoyote duniani pesa zote zitakwenda ndani ya klabu ya Yanga, Makambo hakuchukuliwa kwa mkopo bali tuliingia mkatabanaye wa miaka miwili tukiwa na makubaliano kila kinachoendelea timu yake ya zamani ya Congo inapaswa kujua.”

”Makambo sio mchezaji wangu ni mchezaji wa Yanga na anawakala wake ila aliniomba nimsaidie tu maana mawakala wengi ni wezi wanajua kuwadanganya watoto, ndiyomaana Makambo akaniambia kocha wananiita huku niende unaweza kunisaidia.”

”Kwasababu hakukua na mechi nikamuambia sawa naweza kwenda na nikakuonyesha vitu vyote kama hapa watakuzulumu, mawakala wanajua watoto wengi hawana uzoefu kwahiyo huwazulumu kwakuwa wanajiangalia wao tu wenyewe na sio maslahi ya mchezaji.”

”Akaniambia kama ntaweza kwenda nimwambie ili awaambie kocha wangu anakuja kuangalia mkataba, ili wasimzulumu.”

”Ninachoweza kuwaambia Wanayanga kama timu inamuhitaji tunamuachia kwasababu wanakwenda kumlipa mara tano ya mshahara anaopata hapa, mfano sisi tunamlipa mchezaji sh 100 wakati timu nyingine wanakwenda kumlipa sh 700 huwezi kufanya kitu chochote kwa mchezaji, yeye mwenye ndiyo anaangalia na kufanya maamuzi.”

”Kama Makambo anapata bahati ya kwenda na sisi Yanga tunapata pesa za kutusaidia, kama mimi namlipa mchezaji sh 1000 wakati huko analipwa sh 7000 mimi siwezi kumkataza mchezaji kwenda haiwezekani.”