Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa ushindi waliyopata pata jana timu ya Biashara United dhidi yao haukustahili yalikuwa maamuzi ya ovyo yaliyofanywa na mwamuzi wa mechi kutokana na mchezaji aliyepachika bao hilo alikuwa ameotea ‘Offiside’.Mwinyi Zahera ameyasema hayo katika mahojiano yake na Azam Tv mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, huku akiongeza kuwa bodi ya ligi ilimtumia barua ya yeye kwenda kusema mambo ambayo anayasema, huku akiompongeza Rais Mkuu kutokana na mambo anayosema.

”Unajua kila mara nikisema, wanasema Zahera anafanya hivi mara anafanya hivi. Watu wa bodi ya ligi ya TFF walinitumia barua niende kule nikaseme haya mambo ninayoyasema.”  Zahera ameiyambia Azam tv

Mwinyi Zahera kocha raia wa Congo ameongeza ”Ukiangalia haya mambo yanayotokea hapa, mpira unaonekana Rwanda, Congo na Uganda hivi nivitu vya haya (haibu) vitu vya ovyo mimi siwezi kuficha vitu vya ovyo kama hivi. Mwamuzi sijui kama alikunywa pombe.”

Alipoulizwa na mwandishi wa habari kama anadhani ameonewa kutokana na maamuzi yalityotolewa uwanjani Zahera amesema.

”Lile goli unalionaje wewe, unalionej ?, mtu kaotea ‘offiside’ mita mbili hivi ni vitu vya ovyo mpira hauwezi kuendelea hivi.”

”Rais wenu, rais wenu Mkuu anasema mambo makubwa sana, makubwa sana Afrika nzima, viongozi wengi wamekosa rais wenu. Afrika tuko juu sana sana kutokana na rais wenu.”

Kumewahi kuwa nataarifa kuwa Mwinyi Zahera alitakiwa kwenda kupeleka malalamiko yake TAKUKURU chombo ambacho kinahusika kupambana na rushwa nchini kutokana na kuishutumu Simba kubebwa na hata kutumia pesa.