Baada ya kufanikiwa kupata viongozi wapya kupitia uchaguzi wake mkuu uliofanya Mei 5, 2019, klabu ya Yanga imeanza kuunda safu ya wajumbe wa kamati ya utendaji.

Kamati ya Utendaji kwa kutumia mamlaka iliyopewa na Ibara ya 28 (1) (d) ya Katiba ya Yanga ya mwaka 2010, imefanya uteuzi wa wanachama kuwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga.

Wajumbe wawili walioteuliwa na Kamati ya utendaji ni Dkt. Athumani Kihamia ambaye ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)

Mwingine ni CPA Shija Richard Shija ambaye ni Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Uteuzi huo unaanza mara moja.

Katiba hiyo imetoa mamlaka kwa Kamati ya Utendaji ya Yanga kufanya uteuzi wa wajumbe watatu wa Kamati ya Utendaji.

Aidha taarifa ya klabu hiyo imebanisha kuwa uteuzi wa mjumbe mmoja aliyesalia ili kukamilisha wajumbe watatu utafanyika baadaye.