Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu, ameshindwa kufika mahakamani kwa ajili ya kuhudhuria kesi inayomkabili ya kusambaza picha za ngono kupitia mitandao ya kijamii ambapo wakili wake ameeleza kuwa mshtakiwa huyo ni mgonjwa.Hali hiyo imeelezwa mahakamani leo Jumanne Mei 14, 2019 na wakili anayemtetea Wema Sepetu, Ruben Semwanza ambapo amesema mteja wake ameshindwa kwakuwa ni mgonjwa.Wakili Semwanza amesema,”taarifa nimepewa asubuhi hii nikiwa hapa mahakamani na mdhamini wake hayupo amenieleza yupo kikazi mkoani Arusha, hivyo naiomba Mahakama hii ipange tarehe nyingine,” amedai Semwanza.Kwa upande wake Wakili wa Serikali, Grory Mwenda amedai kuwa shauri hilo lipo kwa ajili ya kusikilizwa pia shahidi aliyetakiwa awepo kutoa ushahidi.

Kesi hiyo imeahirisha kesi hiyo hadi Juni 11, 2019.