Baadhi ya madaktari na watoa huduma za afya wakionesha stika watakazobandika kwenye ofisi zao, mara baada ya kushiriki mafunzo ya siku tano ya namna ya kufanya tahmni ya ugonjwa na ajali zitokanazo na kazi mjini Morogoro. Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) yamefungwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mei 10, 2019. 
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Franck Jacob, (wapili kushoto), akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki Dkt. George mwishoni mwa mafunzo hayo. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini WCF, Dkt.Abdulsalaam Omary, na Daktari bingwa na mbobezi wa magonjwa ya mifupa na viungo, Dkt. Robert Mhina ambaye ni kiongozi wa jopo la watoa mada.


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge, (kulia), akimkabidhi stika, Dkt.Emmanuel M. Shija, kutoka Hospitali ya Rufaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge, (kulia), akimkabidhi stika, Bi. Rosemary K. Mbaule kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini WCF, Dkt.Abdulsalaam Omary, akitoa hotuba ya utangulizi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufunga mafunzo hayo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Frank Jacob, akitoa hotuba yake ya kufunga mafunzo hayo. 
Dkt. Frank Jacob, (wapili kushoto), akibadilishana mawazo na Meneja wa Huduma za Tiba na Tathmini (WCF), Dkt. Ali Mtulia, (watatu kushoto), Dkt. Robert Mhina, (wakwanza kushoto), kiongozi wa jopo la watoa mada, na Dkt. Hussein Mwanga Mhadhiri MUHAS.
Dkt. Pascal Magessa kutoka WCF, akitoa mada juu ya namna ya ulipaji Fidia.
Dkt. Pascal Magessa kutoka WCF, akitoa mada juu ya namna ya ulipaji Fidia. 
Dkt. Pascal Magessa kutoka WCF, akitoa mada juu ya namna ya ulipaji Fidia.
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na washiriki kutoka Dar es Salaam 
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na watoa mada.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Morogoro.

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) tayari umeweza kumetoa mafunzo kwa madaktari na watoa huduma za afya 856 Tanzania Bara kuhusu namna ya kufanya tathmini ya ugonjwa na ajali zitokanazo na kazi

Akizungumza muda mfupi kabla ya kumkaribisha Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kufunga mafunzo ya wiki moja kuhusu namna ya kufanya tathmini hiyo mjini Morogoro Mei 10, 2019, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdulsalaam Omary alisema idadi hiyo ni kuanzia mwaka 2015 tangu Mfuko huo uanze kutekeelza majukumu yake hadi kufikia Mei 10, 2019.

Alisema washiriki waliohudhuria mafunzo ya Morogoro wanatoka mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam na Morogoro na licha ya kufundishwa namna ya kufanya tathmini washiriki pia walifundishwa shughuli za Mfuko ili wao nao wawe mabalozi pindi watakaporejea kwenye vituo vyao vya kazi.

Akifunga mafunzo hayo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Frank Jacob. Aliushukuru Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa kutoa elimu hiyo kwani itasaidia sana kuongeza uwezo wa madaktari katika kutekeleza jukumu hilo kubwa la kufanya tathmini kwa mfanyakazi aliyeumia au kuugua kutokana na kazi.

“Nahakika katika kipindi hiki mlichokuwepo hapa mtakuwa mmejifunza mambo mengi mapya na kuwapa ujuzi ambao huenda hamkuwa nao wakati mnakuja hapa.” Alsiema Dkt. Jacob.

“Mimi toka nimeanza kufanya kazi ya udaktari nina miaka 15 lakini ukiniuliza namna gani unaweza kufanya tathmini kwa mtu aliyepata ajali maeneo ya kazi bado nilikuwa Napata shida, nilikuwa najikanyaga kanyaga sikuwa na uelewa kuhusiana na tathmini ya watu waliopata ulemavu katika maeneo ya kazi.”Alisema.