Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay pamoja na Mkurugenzi  mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela wakati alipowasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, kwa ufunguzi wa Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika katika ukumbi wa Simba, AICC jijini Arusha leo. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati alipowasili katika ufunguzi wa Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC jijini Arusha. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo, Ally Laay.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay wakati alipowasili katika ufunguzi wa Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC jijini Arusha. Katikati ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichele aliyemuwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa wakati alipowasili katika ufunguzi wa Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC jijini Arusha.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC jijini Arusha.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichele akitoa hotuba kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango, wakati wa ufunguzi wa Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC jijini Arusha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC jijini Arusha.