Serikali imewataka wamiliki wa maduka kadhaa ya kubadilishia fedha za kigeni yaliyosimamishwa kuwa watulivu kwa sababu baada ya muda mfupi ujao wataruhusiwa kuendelea na biashara hiyo.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokuwa akifungua semina ya wanahisa wa Benki ya CRDB ikiwa ni sehemu ya mkutano mkuu wa 24 za benki hiyo.

“Wamiliki wa maduka ya kubadili fedha yaliyofungwa wawe watulivu. Benki Kuu inakamilisha utaratibu kabla ya kuwaruhusu waendelee na biashara na kuwahudumia wateja wao,” alieleza Waziri Mkuu.

Utakumbuka kuwa serikali ilifanya ukaguzi wa kushtukiza katika maduka kadhaa katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na dar es Salaam na mengi kufungwa kwa maelezo kuwa yalikuwa yakifanya kazi kinyume cha sheria.