Kutokana na ongezeko la matangazo mengi ya dawa za kuongeza nguvu za kiume na matatizo ya uzazi, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Joseph Kakunda, amewashauri Watanzania kula korosho kwa sababu zina virutubisho vya kurudisha heshima ya ndoa kwa wanaume.Mhe. Kakunda amesema anashangazwa na Watanzania kutokuwa na desturi ya kula korosho ile hali zina virutubisho safi vyenye kuimarisha unyumba.Kakunda ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Mei 16, kuwaelezea maendeleo ya ununuzi wa korosho, ambapo pamoja na mambo mengine amesema hata watu wa mikoa ya kusini wanazaliana sana kwa sababu wanakula korosho kwa wingi

“Korosho ni kirutubisho kizuri, ni ajabu Watanzania hawataki kuzitumia, zinaongeza virutubisho, na kuongeza heshima ya ndoa.” amesema Waziri Kakunda kwenye mkutano wake na waandishi wa habari Jana Mei 16, jijini Dodoma.

Kwenye mkutano huo Waziri Kakunda alikuwa akielezea maendeleo ya ununuzi wa korosho, ambapo pamoja na mambo mengine amesema hata watu wa mikoa ya kusini wanazaliana sana kwa sababu wanakula korosho kwa wingi.