Wanaume wapatao watatu wenye silaha wamevaimia hoteli ya kifahari huko Gwadar katika jimbo la Balochistan, utawala wa nchi hiyo umeeleza.

Vikosi vya usalama vimelizunguka eneo la hoteli hiyo ya ' Pearl Continental'katika mji wa Gwadar baada ya shambulio lililofanywa na watu watatu wenye silaha. Gazeti la Dawm limeripoti.

'Pombe ilinitenganisha na mama yangu'
Kim Kardarshian na Kanye wapata ''mtoto wa nne''
Milio ya risasi ikiwa inaendelea kusikika kutokea ndani ya hoteli. Ripoti kamili inayoeleza idadi ya wageni waliokolewa bado haijatoka.

Mji huo ambao ni kituo cha mabilionea wa uwekezaji wa miradi kutoka China.

Aidha hoteli hiyo inatajwa kuwa na wageni wengi kutoka nje ya nchi ambao ni watalii na wafanyabiashara, lakini bado haijajulikana ni wangapi walikuwa katika hoteli hiyo.


Mashambulio ya aina hiyo ni mengi katika jimbo la Balochistan, eneo ambalo ni la watu maskini zaidi katika nchi hiyo ya Pakistani.