Watu 16 wameshitakiwa nchini Bangladesh kuhusiana na mauaji ya kushtusha ya msichana ambaye alichomwa moto hadi kufa baada ya kuripoti unyanyasaji wa kingono

Nusrat Jahan Rafi, aliyekuwa na umri wa miaka 19, alimwagiwa mafuta ya taa na kuchomwa moto juu ya paa la shule ya kiislamu tarehe 6 Aprili, siku kadhaa baada ya kuripoti unyanyasaji wa kingono

Mwalimu mkuu wa shule yake Siraj Ud Doula, ambaye alidaiwa kumfanyia unyanyasaji huo ni miongoni mwa washitakiwa.

Polisi wanasema aliagiza mauaji yake alipokuwa gerezani wakati alipokataa kuondoa mashtaka dhidi yake.

Walielezea maandalizi ya mauji yake kuwa yalikuwa sawa na "mpango wa jeshi".

Nusrat, ambae alikuwa na umri w amiaka 19, alikuwa anatoka katika mji mdoto wa Feni, uliopo maili 100 kutoka mji mkuu Dhaka. Alikuwa anasoma katika shule ya Kiislamu ya madrassa, tarehe na 7 Machi alisema kuwa Mkuu wa shule alimuita ofisini kwake na kumtomasa. Kabla mambo hayafika mbali alikimbia nje ya ofisi.

Wasichana wengi na wanawake wenye umri mdogo nchini Bangladesh huamua kunyamaza kimya wanapofanyiwa unyanyasaji wa kingono au kubakwa kwa kuhofia kudhalilisha na jamii au familia zao . Kilichomfanywa tofauti na Nusrat Jahan ni kwamba hakuzungumzia suala hilo kwa sauti tu bali - alikwenda pia kwa polisi kwa msaada wa familia yake katika siku ambayo unyanyasaji huo ulidaiwa kufanyika.

Katika kituo cha polisi mjini humo alieleza mashtaka. Alitakiwa kupewa mazingira salama ili aweze kuthathmini yaliyomtokea. Badala yake alichukuliwa video na afisa wa polisi husika kupitia simu yake huku akielezea yaliyompata.

Wanawake wanaofanya kazi wakati wa Ramadhan
Mwili wa Savimbi wazozaniwa
'Roho Mtakatifu' amuepusha dereva na faini
Katika video hiyo Nusrat anaonekana wazi akiwa na mkanganyiko huku akijaribu kuficha uso wake kwa mikono. Polisi anasikika akisema malalamiko hayo "sio jambo kubwa " na kumueleza nusrat aondoe mikono usoni . Baadaye video hiyo ilivifikia vyombo vya habari nchini humo.

Nusrat Jahan Rafi alikuwa anatoka katika mji mdogo, na alizaliwa katika familia yenye ya kihafidhina, na akasomea katika shule ya dini. Kwa msichana kama yeye, kuripoti unyanyasaji wa kingono ni jambo linalokuja na madhara . mara nyingi waathiriwa hukabiliwa na hukumu kutoka kwa jamii zao, udhalilishwaji wa moja kwa moja na kupijtia mtandao , na wakati mwingine hupigwa. Nusrat alikabiliwa na yote haya.

Tarehe 27 Machi, baada ya kwenda polisi, walimkamata mwalimu wake mkuu. Baada ya hapo mambo yakaanza kuwa mabaya kwa Nusrat. Kundi la watu walikusanyika kwenye mitaawakidai aachiliwe. Waandamanaji walikuwa wamekusanywa na wanafunzi wawili wa kiume na wanasiasa wa eneo hilo wanaripotiwa kuwa walihudhuria maandamano hayo . Watu walianza kumlaumu Nusrat. familia yake inasema ilianza kuhofia usalama wake.

Licha ya hayo , tarehe 6 Aprili, siku 11 baada ya unyanyasaji huo unaodaiwa, Nusrat alikwenda shuleni kwake kufanya mitihani yake ya mwisho.

"Nilijaribu kumchukua dada yangu shuleni na kujaribu kuingia shuleni, lakini nikazuwiwana sikuruhusiwa kuingia ," alisema kaka yake Nusrat, Mahmudul Hasan Noman.

"Nisingezuwiwa, jambo kama hili lisingemtokea dada yangu ," alisema.

Kwa mujibu wa taarifa ya mashtaka iliyotolewa na Nusrat, mwanafunzi mwenzake wa kike alimpeleka kwenye paa la shule, alisema mmoja wa marafiki zakealikuwa amechapowa . Wakati Nusrat alipofika juu ya paa watu wanne au watano, waliokuwa wamevalia burqa, walimzingira na kumshinikiza aachane na kesi dhidi ya mwalimu mkuu. Alipokataa ndipo walipomwagia mafuta ya taa na kumchoma kwa moto.

Mkuu wa Idara ya upelelezi ya polisi Banaj Kumar Majumder alisema kuwa wauaji wanaotafutwa "walitaka kufanya mauaji hayo yaonekane kama Nusrat alijiua mwenyewe ". mpango wao uliharibika wakati Nusrat alipookolewa baada baada ya kutoroka eneo la tukio. Aliweza kutoa taarifa kabla ya kufa.


Umati mkubwa wa watu ulikusanyika katika mji alikozaliwa Nusrat wa Fenkuhudhuria mazishi yake
" Mmoja wa wauaji wake alishindilia kichwa chake chinikwa kutumia mikono yake, kwa hiyo mafuta ya taa hayakumwagika palena ndio maana kichwa chake hakikuungua ," Bwana Majumder aliiambia BBC mjini Bengali.

Lakini wakati Nusrat alipopelekwa katika hospitali iliyopo karibu majeraha mwili wake ulikuwa na 80% ya majeraha ya mwili wake . Hawakuweza kutibu vidonda , na kuamua kutuma katika hosptali ya chuo cha tiba cha Dhaka.

Alipokuwa katika ambilansi, kwa kuhofia kuwa hatapona, alirekodi taarifa katika simu ya mkononi ya kaka yake.