Wakenya wamekuwa wakitumia mtandao wa kijamii wa Twitter kuuliza maswali kuhusu mahali aliko rais wao Uhuru Kenyatta. Bw. Kenyatta aliondoka nchi humo Aprili 23 kukutana na mwenzake Xi Jinping nchini China na inasadikiwa kuwa alirejea nyumbani kimya kimya Mey 3. Kwa mujibu wa gazeti la The Standard. Kutoonekana hadharani kwa rais Kenyatta kumezua gumzo katika mitandao ya kijamii, huku wanasiasa wakipeana sababu tofauti kwa nini wanadhani raia ameamua kuwa kimya.Kwa mujibu wa BBC. Gavana wa jimbo la Machakos lililopo nje kidogo ya mji mkuu wa Nairobi, Dr. Alfred Mutua alinukuliwa na vyombo vya habari akimtetea rais kwa kutoonekana hadharani kwa mda.

”Rais ni meneja mwenye shughuli nyingi kwa hiyo anahitaji mmda wa kufanya mikutano, kupokea taarifa muhimu za serikali na kushughulikia masuala ya uchumi wa nchi” alisema Bw. Mutua.

Aliongeza kuwa anashangaa kusikia watu wakiulizia kwanini rais hajaonekana hadharani tangu arejee kutoka ziara ya China.

Hata hivyo kupitia hashtag ya #FindPresidentUhuru, wakenya katika mtando wa kijamii wa Twitter maarufu KOT walituma ujumbe wa kutaka kujua rais Kenyatta yuko wapi.

View image on Twitter
View image on Twitter

K24 TV

@K24Tv
 #FindPresidentUhuru KOT launches operation to find 'missing' president.  #K24Alfajiri w/ @SerahTeshna, @iamjeffmote and @mungalambuvi,

12
7:20 AM - May 13, 2019 · Kenya
See K24 TV's other Tweets
Twitter Ads info and privacy
Baadhi yao walijaribu kuelezea kwanini rais hajaonekana hadharani kwa majuma mawili.

Wengine wanadai kuwa rais kwanza alifuta akaunti zake rasmi za mitandao ya kijamii na kisha akaelekea ziara ya China kutafuta mkopo. Hivyo ndivyo rais wetu alivyotoweka! Yuko wapi Uhuru Kenyatta? walimalizia kwa kuuliza sawali hilo.


Mr maurice njiriri
@morrisnjiriri
 ðŸ¤£ðŸ¤£ðŸ¤£ðŸ¤£RT @Waambui: Maybe Uhuru is hiding from auctioneers and you people are out here shouting #FindPresidentUhuru.

It's better that you don't know his whereabouts. You are those kids of "amesema hayuko" 😂😂😂

13
6:58 PM - May 12, 2019
Twitter Ads info and privacy
See Mr maurice njiriri's other Tweets
Maneno kama vile Hashtags, tweets, retweets na memes hutumiwa sana katika mtandao wa kijamii wa Twitter.

Watu wengi walio na miaka zaidi ya 40 huenda wasiwa na ufahamu kuyahusu lakini maneno hayo huwaleta pamoja jamii ya wakenya inayofahamika kama KOT katika mtandao wa Twitter.

@ItsMutai aliandika katika Twitter yake kuwa ”Rais Uhuru Kenyatta amepotea tangu aliposafiri kwenda, China. Hakuna mtu yeyote aliye na taarifa ya juu ya kuonekana kwake hadharani. Ukiona ujumbe huu tafadhali, retweet ili utusaidie #FindPresidentUhuru. Wakenya hawastaili kukosa kumuona rais wao kwa zaidi ya saa 24 . Umemwona mahali? Tuambie.”

“Ndugu yake Raila atuthibitishie ikiwa rais Kenyata hakurudi nchini baada ya ziara ya China,” aliandika @MoyalePundit.

Licha ya hashtag ya #FindPresidentUhuru, kusbaa katika mitandao ya kijamii kuanzia siku ya Jumamosi kitengo cha mawasiliano cha rais Kenyatta hakijatoa tamko lolote.

Hashtag zinazohusiana na masuala ya kisiasa sio maarufu kuliko masuala mengine ya kijamii, lakini hashtag ya #Kenya@50 ilitajwa kuwa miongoni mwa hashatag maarufu za kisiasa barani Afrika.