Muungano wa upinzani nchini Sudan pamoja na makundi ya waandamanaji, wameshiriki mgomo kulishinikiza baraza la jeshi kuachia madaraka utawala wa kiraia.
Kwa mujibu wa shirika la habari la nchini Ujerumani DW, Wahudumu wa afya, umeme na wafanyakazi wa benki walishiriki mgomo huo na katika sekta nyingine shughuli ziliathiriwa kidogo.
Kufuatia mgomo huo, baadhi ya mashirika ya ndege yalisitisha safari zao kutoka uwanja wa ndege wa Khartoum.
Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa mamia ya wasafiri walikwama katika uwanja wa ndege mjini Khartoum na katika baadhi ya vituo vya mabasi.
Kama hatua ya kuongeza shinikizo dhidi ya baraza la kijeshi linaloshikilia madaraka kwa sasa, vuguvugu linaloendesha maandamano kwa jina Freedom and Change, limeitisha mgomo wa kitaifa wa siku mbili kuanzia leo.