Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
WAFANYABIASHARA wadogo na wauzaji wa vifungashio na mifuko mbadala wameiomba Serikali kutoa maelekezo maalumu ni wapi watapata mifuko mbadala baada ya matumizi ya mifuko ya plastiki kusitishwa kuanzia Juni mosi mwaka huu.

Wakizungumza  na Blogu ya jamii kwa nyakati tofauti wafanyabiashara katika soko la Kariakoo jijiji Dar es Salaam wamesema kuwa wamelipokea suala hilo kwa mikono miwili kwa kuwa matumizi ya mifuko ya plastiki athari zake zimeonekana hivyo ni vyema kutumia mifuko mbadala iliyoelekezwa ili kutunza mazingira.

Aidha wamesema kuwa upatikanaji wa mifuko mbadala ya kwa wafanyabiashara hao Mkuu wa Wilaya hiyo Sophia Mjema tayari ametoa maelekezo ya wapi vifungashio na mifuko mbadala itapatikana kabla ya tarehe elekezi.

Aidha wameiomba serikali kuzidi kutoa elimu ya uelewa juu ya athari za mifuko ya plastiki katika mazingira ili kila mmoja awe sehemu ya utunzaji wa mazingira.

Kwa upande wao akina mama wanaofanya biashara za kuuza unga wa lishe, korosho na ubuyu katika soko la Mwenge jijini humo wameiomba serikali kutoa maelekezo ya kina ni mifuko ipi haitakiwi kimatumizi, na kuiomba kuelekeza mifuko mbadala ambayo itafaa katika uhifadhi wa bidhaa hizo kwa ubora zaidi.

Vilevile kwa upande wa wauzaji wa vifungashio na mifuko mbadala wamesema kuwa mifuko na vifungashio hivyo vinapatikana Mikoani hasa katika Mikoa ya Lindi, Mtwara, Lindi na nchi jirani ya Kenya ambapo usafiri na kodi ni kubwa na wameiomba serikali kuangalia suala hilo hasa kwa kuhakikisha viwanda vya kutengeneza vifungashio na mifuko mbadala vinapatikana kwa wingi nchini.
 Muuzaji wa vifungashio na mifuko mbadala Benjamin Paul akizungumza na blogu ya jamii kuhusiana na usitishwaji wa mifuko ya plastiki ambapo ameiomba serikali kuangalia na kuwekeza katika viwanda vya ndani ambavyo vinazalisha mifuko hiyo.
Mjasiriamali wa unga wa lishe na korosho Mariam Seif akizungumza na Michuzi blogu kuhusiana na matumizi ya mifuko mbadala ambapo ameiomba serikali kutoa elimu na maelekezo zaidi juu ya mifuko iliyokatazwa. 
 Baadhi ya vifungashio mbadala ambavyo vinaruhusiwa kimatumizi kuanzia June Mosi.
Muuzaji wa mifuko ya plastiki Alawi Zeni akizungumza na blogu ya jamii kuhusiana na katazo la mifuko ya plastiki na kueleza kuwa wapo tayari katika kushiriki kukomesha matumizi ya mifuko hiyo.