Wachungaji watatu kutoka KKKT DMP na mmoja kutoka KKKT Dayosisi ya Ziwa Victoria Shinyanga Wamehitimu katika Chuo Kikuu cha Luther Seminary Minnesota nchini Marekani tarehe 19/05/2019 kama ifuatavyo:- Rev. Dr. Ernest William Kadiva ametunukiwa Phd - Doctor of Ministry, Wengine wametunukiwa Master of Arts degree nao ni Rev. Kishe Dismas Mhando - na Rev. Kaanasia Geofrey Msangi, pia Rev. Martha Ernest Ambarang'u wa Dayosis ya Ziwa Victoria Shinyanga ametunukiwa Masters of Arts degree katika mahafali ya 150 iliyofanyika hapa Central Lutheran Church, Minneapolis na kuhudhuriwa na mamia ya wageni kutoka nchi mbalimbali na kutoka majimbo mbalimbali ya Marekani. Picha kwa hisani ya Noah William Kadiva akiwa Minnesota, Marekani.
Ndugu, jamaa na marafiki wakifurahia baada ya Rev. Dr. Ernest William Kadiva kutunukiwa Phd - Doctor of Ministry, na wengine waliotunukiwa Master of Arts degree Rev. Kishe Dismas Mhando - na Rev. Kaanasia Geofrey Msangi, pia Rev. Martha Ernest Ambarang'u wa Dayosis ya Ziwa Victoria Shinyanga 
Rev. Dr. Ernest William Kadiva akitunukiwa Phd - Doctor of Ministry baada ya kuhitimu katika Chuo Kikuu cha Luther Seminary Minnesota kwenye sherehe zilizofanyika Central Lutheran Church, Minneapolis, nchini Marekani.