Shirikisho la soka nchini, TFF, limetangaza bei za viingilio kwa mchezo wa kimataifa utakaowakutanisha mabingwa wa Tanzania Bara, Simba SC na Sevilla FC kutoka nchini Hispania.Mechi hiyo ya kukata na shoka inatarajiwa kupigwa siku ya Mei 23 kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia majira ya saa 1:00 Usiku.Akizungumza kwa niaba ya TFF, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa shirikisho hilo, Ndugu Cornel Barnaba ametangaza bei za tiketi kuelekea mchezo huo.