Vifurushi vya Huawei vyasafirishwa kwa makosa
Kampuni ya FedEx ya Marekani nchini China, leo imetoa taarifa ikisema baadhi ya vifurushi vya kampuni ya Huawei vimesafirishwa kwa makosa. Kauli hiyo ni tofauti na taarifa zilizotolewa kwenye mtandao wa kijamii wa Weibo siku chache zilizopita.

Habari mpya zinaonyesha kuwa, kampuni ya Huawei imetoa malalamiko kwa idara ya usimamizi wa posta ya China kuhusu tukio hilo.

Habari kutoka shirika la habari la Reuters Mei 24 mwaka huu zilisema, vifurushi viwili vya Huawei ambavyo vinasambazwa na Fedex kutoka Japan kwenda China vimesafirishwa kwenda Marekani, na Fedex pia inajaribu kusafirisha vifurishi vingine viwili vya Huawei kutoka Vietnam kwenda Marekani, ambavyo vingekwenda kwenye ofisi za sehemu nyingine za Asia.