*Bilioni 55 zatolewa ili kuwajengea vijana ujuzi

AWAMU ya kwanza  ya programu ya kuwasaidia vijana nchini katika kuboresha maisha yao kupitia programu za kuimarisha ujuzi imezinduliwa rasmi leo huku shirika la maendeleo na ushirikiano la Uswisi (SDC) likitoa shilingi bilioni 55 kwa kipindi cha miaka 12 katika kuboresha maendeleo ya mafunzo ya ufundi stadi nchini Tanzania.

Akizungumza katika warsha hiyo ya uzinduzi Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa mafunzo hayo yatanufaisha vijana wengi na takribani vijana 15,000 watafikiwa na mafunzo hayo huku akieleza kuwa kupitia sekta ya elimu vijana watapata nafasi ya kujifunza kilimo bora na cha kisasa ili kutengeneza ajira nyingi zaidi.

 Amesema kuwa mradi huo utakuwa karibu na sekta binafsi ili kuwawezesha vijana kupata ajira huko, na kusisitiza  kuwa mafunzo yanayotolewa lazima yaendane na mfumo wa soko la sasa na kuwa kupitia mradi huo wataboresha mifumo ya ufundishaji na ujifunzaji kwa vyuo 16 vya maendeleo ya wananchi ili kuweza kuendana na mafunzo ya kiteknolojia na hiyo ni kutoa mafunzo kwa wakufunzi  ili waweze kuwanoa wanafunzi na kuwafanya wawe wabobezi katika ujuzi wa fani wanazozisomea tangu wakiwa shuleni.

Vilevile ameishukuru Serikali ya Uswisi kwa ushirikiano waliouonesha kwa serikali kwa kutoa bilioni 55 za kuendeleza ujuzi na vijana kupata ajira au kuajirika kwa urahisi zaidi na amehaidi kuwa watanzania wengi wafanufaika na mradi huo.

Kwa upande wake Balozi wa Uswisi nchini Florence Tinguely Mattli amesema kuwa programu hiyo ni mkakati wa taifa wa maendeleo ya stadi na ufundi mkakati unaolenga kuimarisha na kukuza fursa za maendeleo ya stadi zinazotokana na mahitaji ya ajira, huku akieleza matarajio makubwa ya programu hiyo nchini ni kuendeleza ujuzi na kuwawezesha vijana kujiajiri na kuajiriwa kirahisi zaidi.

Balozi Mattli amesema kuwakupitia programu hiyo watashirikiana na sekta binafsi pamoja na  vyuo vya mafunzo stadi VETA ili kuweza kuyafikia malengo yaliyowekwa kwa urahisi zaidi huku wanawake wakipewa kipaumbele zaidi na kuahidi kuwa kupitia mafuzo hayo watanzania wajiandae kupokea huduma bora zenye viwango bora zaidi na hiyo ni kupitia kauli mbiu ya Hapa Kazi Nzuri Tu!

Uswisi imekuwa na ushirikiano mkubwa na serikali ya Tanzania  na imekuwa ikichangia katika kuendeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo tangu mwa 1960 kwa kutoa shilingi bilioni 51 kila mwaka katika kusaidia sekta za elimu, afya, kilimo, utawala bora, ajira na mapato.
Balozi waUswisi nchini Florence Tinguely Mattli  akizungumza kuhusu programu ya kuwasaidia vijana nchini katika kuboresha maisha yao kupitia programu za kuimarisha ujuzi huku shirika la maendeleo na ushirikiano la Uswisi (SDC) likitoa shilingi bilioni 55 kwa kipindi cha miaka 12 katika kuboresha maendeleo ya mafunzo ya ufundi stadi nchini Tanzania iliyofanyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya kuwasaidia vijana nchini katika kuboresha maisha yao kupitia programu za kuimarisha ujuzi huku shirika la maendeleo na ushirikiano la Uswisi (SDC) likitoa shilingi bilioni 55 kwa kipindi cha miaka 12 katika kuboresha maendeleo ya mafunzo ya ufundi stadi nchini Tanzania.
Profesa Samuel Wangwe akiwasilisha mada wakati wa uzinduzi wa programu ya kuwasaidia vijana nchini katika kuboresha maisha yao kupitia programu za kuimarisha ujuzi uliofanyika leo katika ukumbi wa hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wadau wakichangia mada kwenye uzinduzi wa programu ya kuwasaidia vijana nchini katika kuboresha maisha yao kupitia programu za kuimarisha ujuzi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa elimu wakiwa kwenye mkutano wa uzindizi wa programu ya kuwasaidia vijana nchini katika kuboresha maisha yao kupitia programu za kuimarisha ujuzi utakadumu kwa miaka 12 uliofanyika leo katika ukumbi wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja