MUME wa wanamuziki wa miondoko ya mduara Bongo, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, Ashiraf Uchebe amesema yuko kwenye maombi kwa ajili ya kumuombea mkewe ili aendelee kubadilika na kuachana na mambo yasiyompendeza Mungu.  Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Uchebe alisema Shilole wa sasa sio wa zamani na kwa watu waliokuwa wakimjua lazima wanaona kuna mabadiliko makubwa.

“Hata hivyo sijachoka kwa sababu nampenda mke wangu huyu ambaye mimi naona ni zawadi kutoka kwa Mungu, bado nipo kwenye maombi ya kumuombea abadilike kabisa ili arejee kwa Mwenyezi Mungu mazima. Mwanzo nilidhani itakuwa kazi ngumu kumbadili lakini imekuwa rahisi sana na kila kukicha anabadilika,” alisema Uchebe