Rais wa Marekani Donald Trump ametetea vita vya kibiashara kati yake na China wakati hali ya wasiwasi ikiongezeka wakati masoko ya fedha yakizidi kuporomoka huku akiahidi kufikia makubaliano hivi karibuni na rais wa China Xi Jinping.

Katika mfululizo wa ujumbe alioandika kwenye ukurasa wake wa twitter mapema hii leo Trump ameendelea kuipigia debe kauli mbiu yake ya Marekani Kwanza katika kuunga mkono hatua za kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China huku akiyataka makampuni ya Marekani kumuunga mkono kwa kuhamisha biashara zao kutoka China.

Trump amesema kwa sasa anaweza kufikia makubaliano na Beijing lakini hatakubali tena kuwekewa mbinyo huku akiikosoa China kwa jaribio lake la dakika za mwisho la mazungumzo.