Club ya TP Mazembe ambao ni vigogo wa soka Afrika baada ya kuwahi kupata vipaji vya soka vya wachezaji wa kitanzania kama Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu sasa wameamua kurudi tenza Tanzania, TP Mazembe sasa wameripotiwa kuwa mbioni kutaka kumsajili Ibrahim Ajib wa Yanga.Kwa mujibu wa barua iliyoonekana mtandaoni inaeleza kuwa TP Mazembe wanafahamu kuwa mkataba wa Ajib na Yanga unamalizika June 30 lakini wanaomba barua kutoka Yanga SC ya kuonesha kuwa mchezaji huyo anamaliza mkataba wake na wanaweza kumalizana nae