Kwa mujibu wa mtandao wa ‘The Blast’ umeripoti kuwa mwimbaji The Weekend alifunguliwa shtaka na mshairi mwenye asili ya Somali-America kuwa aliibiwa wimbo wake wa “Jewel of My Life” aka “Hooyo,” aliouachia rasmi mwaka 2006 na kupata muitikio mkubwa Afrika.
Mshairi huyo aliyetambulika kwa jina la Yasminah alidai kuwa The Weekend aliachia ngoma yake ya “Starboy” mwaka 2016 na kugundulika kuwa ngoma hiyo inafanana na yake na aliamini kuwa The Weekend alipata kufahamu ngoma yake kwa sababu ilifanya vizuri kwenye jamii ya Afrika Mashariki na hivyo alifungua shitaka na kudai thamani ya shilingi Bilioni 11 za Kitanzania.
Kwa mujibu wa makala kutokea mahakamani umedai kuwa The Weekend amekataa kuhusiana na ishu hiyo na kutaka kesi hiyo kufutwa huku akisema kuwa ngoma yake hiyo ilitungwa kwa umakini na hata hivyo wafanyakazi wenzake walitoa uhuru wakidai kazi hiyo kama imeibiwa.