Aliyewahi kuwa Waziri wa Michezo Zanzibar, Ali Juma Shamhuna amefariki dunia visiwani humo.
Pia Shamhuna aliwahi kuwa Naibu Waziri Kiongozi katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar .
Shamhuna alikuwa ni mtu wa karibu wa marehemu Ali Fereji Tamim (Rais wa zamani wa Chama cha Soka cha Zanzibar - ZFA).