Aliyekuwa msanii wa muziki wa hip hop Bongo na sasa Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi 'Sugu', yeye na mkewe wamejaliwa kupata mtoto wa kiume.

Mbunge huyo ameeleza kuwa mkewe na mtoto hadi sasa wanaendelea vizuri. Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram ameandika;

"Tunamshukuru sana Mungu, usiku wa kuamkia leo tarehe 15 Mei 2019 ametujalia mtoto wa kiume. Mama na mtoto wote wanaendelea vizuri," ameeeleza.

Ameendelea kwa kusema, "Asanteni sana wote hasa kwa maombi na kututakia mema kwenye kipindi chote cha ujauzito wa Happiness. Hakika nina furaha isiyo kifani,".