StarTimes imeendelea kutembelea shule za msingi jijini Dar es Salaam, ikiwa ni katika kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili.
Alhamisi hii walitembelea shule ya Msingi Makuburi Jeshini iliyoko Ubungo jijini Dar es Salaam ambapo wawakilishi wa StarTimes walikutana na kuzungumza na wanafunzi wa darasa la awali hadi darasa la nne kutoka shule hiyo.
Pamoja na kuzungumza na wanafunzi wawakilishi wa StarTimes walitoa zawadi kwa ya king’amuzi na Dish kwa uongozi wa shule na zawadi mbalimbali kwa wanafunzi walioweza kujibu vizuri maswali yaliyoulizwa.
“Asanteni sana kwa kututembelea Shuleni kwetu na kwa zawadi mlizotuletea sisi pamoja na wanafunzi. Mmewapa changamoto wanafunzi wetu lakini pia mmetuonyesha ni wapi tunahitaji kuongeza juhudi katika ufundishaji kwa sababu hapa tumeona watoto wanaelewa zaidi kwa kutazama kama wanavyojifunza kupitia maudhui ya chaneli yenu ya ST Kids.” Mwalimu Mkuu Msaidizi Shule ya Msingi Makuburi Jeshini Mary Antony Manyika.
ST Kids ni chaneli ya kwanza Tanzania ya watoto ambayo vipindi vyake vinapatikana kwa lugha ya Kiswahili, lengo likiwa ni kuwawezesha watoto kuburudika na katuni na maudhui mengine kwa lugha ambayo wanaifahamu vizuri ili kusaidia ukuaji wao miongoni mwa familia na jamii zao.
“Lengo letu kutembelea shule hizi ni kutambulisha maudhui mapya yanayopatikana katika chaneli ya ST Kids ambayo yako katika lugha ya Kiswahili. Vipindi ni vizuri kwa watoto kwani vinawafundisha stadi mbali mbali za maisha.” Dina Marious Balozi wa StarTimes Kids
“Kila Shule tuliyotembelea tunawasikiliza changamoto zao na sisi kama kampuni tutajaribu kuangalia ni namna gani tunaweza kusaidia. Kwa mfano hapa leo wametueleza shule ina changamoto ya maji, hivyo katika mipango yetu ya shughuli za kimaendeleo tutawafikiria pia.”
Kampeni hii ya kutembelea mashule jijini Dar es Salaam itaendelea hadi mwisho wa mwezi wa tano na itafikia jumla ya shule 7 katika Wilaya 3 za Mkoa wa Dar es Salaam.
Chaneli ya ST Kids inapatikana katika kifurushi cha UHURU kilichoboreshwa kwa watumiaji wa dikoda ya Antenna na kuanzia kifurushi cha SMART kwa watumiaji wa dikoda ya Dish.
Mtangazaji wa Efm radio, Dina Marios(kushoto) akimkabidhi zawadi ya dishi na dekoda ya Startimes Mwalimu Mkuu Msaidizi Shule ya Msingi Makuburi Jeshini Mary Antony Manyika wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili.
Mtangazaji wa Efm radio, Dina Marios(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi zawadi ya dishi na dekoda ya Startimes kwenye Shule ya Msingi Makuburi Jeshini wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili.
Mwalimu Mkuu Msaidizi Shule ya Msingi Makuburi Jeshini Mary Antony Manyika akizungumza na waandishi wa habari mara baada mara baada ya Shule ya Msingi Makuburi Jeshini kukabidhiwa zawadi ya dishi na dekoda ya Startimes wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili.