Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kuwa amemuandikia barua Rais wa PAP ya kusitisha uwakilishi wa Stehen Masele hadi Kamati ya Maadili itakapokamilisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake.

Akizungumza leo Bungeni amesema katika jambo hilo kuna kamati mbili zinamsubiri ikiwemo Kamati ya Maadili ya Bunge na Kamati ya Maadili ya chama chake.

"Katika uwakilishi wa Bunge la Afrika kumetokea matatizo makubwa hasa kwa Mhe.Steven Masele matatizo ya kinidhamu,Tumelazimika kumrudisha nyumbani kuanzia Jumatatu, badala yake amekuwa akionyesha kugoma, ni kiongozi ambaye anafanya mambo ya hovyo hovyo ".Spika Ndugai.

Ameendelea kwa kusema, "Stephen Masele ni kiongozi ambaye amekuwa akifanya mambo ya hovyohovyo, ndiyo maana tumemuita atufafanulie huenda yuko sahihi, lakini anafanya mambo ambayo ni hatari kubwa, amekuwa akichonganisha mihimili miwili, ni amejisahau sana'.