Mwanzilishi wa Smart Me App, Innocent Mathias amewataka vijana wenzake kuwa msitari wa mbele kuweka malengo yao katika masomo huku wakijiwekea akiba katika kipato cha fedha wanazopata.
Mwanzilishi mwenza wa Smart Me App, Edgar Luambano akiongea machache.


Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Vijana wa kitanzania watakiwa kuweka utaratibu wa kujiwekea akiba na kujiepusha na matumizi mabaya ya fedha

Akizungumza wakati akitoa mafunzo kwa wanafunzi wa Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kiongozi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya SMART ME Tanzania, Edgar Luambano amesema kuna haja ya kila kijana kujiwekea mazoea ya kuweka akiba.

Amesema vijana wengi wanapomaliza chuo akili na mawazo yao huwa ni kuajiliwa sasa, pindi anapokaa muda mrefu mtaani hujikuta anakosa akiba hata kidogo...hivyo tukianza kuweka hata shilingi 500 kwa siku itawavusha.

"Natoa wito kwa vijana wote hasa walioko vyuoni wajenge tabia ya kuweka akiba kwaajili ya maisha ya baadae huku wakijapanga kukabiliana na madeni ya bodi ya mkopo wa vyuo vikuu (HESLB) na ukosefu wa ajira pindi watakapomaliza chuo,".

Nae Kiongozi mwenza wa Innocent Mathias amesema kuwa Kampeni ya kuweka akiba siku 365 (365 SAVING PLAN CHAMPAIGN) inaendeshwa na SMART Me Tanzania inalenga kusaidia vijana kutokana na utegemezi na janga kubwa la ukosefu wa ajira kupitia akiba.

"Sisi tunaamini katika dunia ijayo inayoongozwa na vijana wasiotegemezi, wenye maamuzi na uchumi hai” amesema Innocent Mathias.

Amesema kuwa kwasasa SMART Me inatarajia kuzindua mfumo wa kuweka akiba kwa kutumia simu (SMART ME Mobile App) itakayo wasaidia vijana kuweka akiba na kutengeneza faida kwaajili ya manufaa yao ya baadae.

Katika tukio hilo taasisi imetoa zawadi kwa washindi wawili wa kampeni ya 356 SAVING PLAN CHAMPAIGN, ambao ni Steven Kivuyo (mshindi wa kwanza) na Ashura Yunus Mussa wote wanafunzi wa IFM ambao wameonyesha uthubutu wa hali ya juu katika kujitengenezea akiba ya fedha kwa wakati huu wakiwa bado wapo chuo.

Tukio hilo liliwashirikisha benki ya NBC pamoja na taasisi ya UNILIFE CAMPUS.