Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mhe. Paul Makonda amesema kwa hapa duniani anaweza kunyanyaswa au kufanyiwa zengwe na binadamu wenzake lakini kwa upande wa kiroho kuna maisha mengine mbinguni ambayo hakuna binadamu wa kumnyanyasa mtu.RC Makonda ametoa kauli hiyo wilayani Arumeru wakati akizungumza na na mamia waliojitokeza kwenye Mazishi ya RCO wa Ilala SSP Anael Mbise.