Kikosi cha Simba kitacheza mchezo wa kufunga Ligi Kuu Bara leo Jumanne dhidi ya Mtibwa Sugar na mara baada ya kumalizika mabingwa hao wa ligi watakabiziwa kombe na zawadi zao za ubingwa.Baada ya mchezo huo kikosi cha Simba kitaanza safari ya kurudi Dar es Salaam Jumatano watakapofika Kibaha wataanza shangwe na sherehe za ubingwa.