VINARA wa soka katika michuano ya Ligi Kuu ya Hispania, LaLiga, timu ya Sevilla FC inatarajiwa kuwasili nchini kesho kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya  Simba ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya  kwa timu hiyo kucheza nchini  Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana jijini  Dar es Salaam, timu hiyo inatarajiwa kuwasili kesho jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius  Nyerere.

Kulingana na taarifa hiyo mechi hiyo itakuwa ni maalum kwa vinara hao wa 'LaLiga ambao wanadhaminiwa na  SportPesa' na akaongeza  kwamba ziara itahusisha matukio kadhaa ya   jamii na michezo ikiwemo kliniki namafunzo mbalimbali.

 "Kama ushindani wa kimataifa unakutana na dhamira ya LaLiga kuwa karibu na mashabiki wake. Kwa kweli kwamba mashabiki wetu wa Tanzania wataweza kupata furasa ya  kuangalia karibu  klabu kubwa kama Sevilla FC inamaanisha kuwa ni fursa kubwa kwa kila mtu," alisema Mkurugenzi wa Maendeleo ya Kimataifa katika Ligi ya La Liga, Oscar Mayo.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Tarimba Abbas, kampuni yao  imeshirikiana na baadhi ya taasisi za soka za kubwa  ulimwenguni  baada ya kuna kuna haja ya  kuleta uzoefu  huu mkubwa  kwa Tanzania.

 "Ili kufurahia kuona moja ya klabu  kubwa za  mpira wa miguu  Ulaya, Sevilla FC. Kwa makubaliano yetu na LaLiga ambayo ni ligi bora duniani, tutaweza kuonyesha vipaji vyetu  na kuboresha kiwango cha soka  nchini ", alisema Talimba.

 Alisema kwamba mechi hiyo ni sehemu ya mradi wa 'LaLiga duniani  ambao unalenga kueneza soka  la  Hispania kimataifa na  kueneza pia sera ya 'Marca EspaƱa', kuleta karibu mashabiki wa  LaLiga na  kukuza klabu nje ya nchi yetu.

Hii itakuwa ni klabu ya pili Ulaya kufanya ziara Afrika Mashariki, baada ya mwaka 2017 Everton FC kucheza  na  Gor Mahia  nchini  Kenya, ingawa  sio mara ya lkwanza kwa  Sevilla kutua katika bara hili kwani  mwaka  2015  ilikuwa nchinbi  Morocco ambao ilicheza mechi ya kuajindaa na  LaLiga dhidi ya timu ya   Hassania Union Sport d'Agadir.