Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu (mwenye hijab mbele), akizunhgumza baada ya zoezi la kuwasha umeme kwenye vijiji vya Muhoro Mashariki na Magharibi wilayani Rufiji Mkoani Pwani leo Mei 22, 2019. Takriban Kata 26 zimefaidika na zoezi hilo.
 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, (aliyesimama), akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kuwasha umeme katika vijiji vya Muhoro Masharki na Magharibi iliyofanyika shule ya msingi Nyampapu wilayani Rufiji Mkoani Pwani leo Mei 22, 2019. Mwenye shati la bluu ni Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Mhe. Juma Njwayo.
 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, (wapili kulia), akiongozana na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Rufiji baada ya hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, (kushoto), akipokea zwadi kutoka kwa akina mama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), baada ya kuhutubia wananchi katika hafla ya kuwasha umeme iliyofanyika shule ya msingi Nyampapu iliyopo Muhoro Mashariki wilayani Rufiji Mkoani Pwani leo Mei 22, 2019. (PICHA NA SAMIA CHANDE).

NA SAMIA CHANDE, RUFIJI.

NAIBU Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu amewasha umeme katika vijiji vya Muhoro Mashariki na Magharibi wilayani Rufiji Mkoani Pwani leo Mei 22, 2019 ikiwa ni muendelezo wa Serikali kuhakikisha watanzania wote wakiwemo wa vijijini wanapata umeme.


Akiwaelimisha wananchi kuhusu gharama za kuunganishiwa umeme wakati wa hafla hiyo iliyofanyika shule ya msingi Nyampapu iliyoko kijiji cha Muhoro Mashariki, Naibu Waziri alisema serikali inaowajibu wa kumlinda mlaji na mtumiaji wa huduma mbalimbali ndio maana katika swala la umeme vijijini imeshusha gharama za kuunganishiwa umeme hadi shilingi 27,000/= tu.


 “Awali gharama za kuunganishiwa umeme zilikuwa ni shilingi 177,000, lakini Serikali kwa vile inawajali wananchi wake imelipa shilingi 150,000/= kwa kila anayeweka umeme, na kazi ya mwananchi ni kulipia kiasi kidogo tu cha shilingi 27,000/=, tofauti na hapo awali.” Alisema Mhe. Naibu Waziri Mgalu katika hafla hiyo ambapo takriban Kaya 26 zimefaidika na zoezi hilo.


Alisema anatambua wapo wananchi wapo karibu na miundombinu ya njia ya umeme na sio kwamba wanashindwa kulipa shilingi elfu 27,000/= bali wanashindwa na gharama ya kutandaza umeme ndani ya nyumba (wiring) inayofanywa na wakandarasi.(mafundi).


“Alisema gharama hizo za wiring zimeonekana kuwa ndio changamoto kwa wananchi na serikali imepokea changamoto hiyo na kwamba itafanyia kazi.” Alisema.
Alitoa wito kwa wakandarasi wanaofanya kazi ya wiring wazingatie vipato vya watanzania wenzao, watakapoweka bei kubwa watapata wateja wachache lakini wakiweka bei ya kawaida, wateja wengi ambao serikali imelenga kuwaunganishia umeme watawapata.


Aidha Mhe. Naibu Waziri Subira Mgalu, aliwataka wananchi wa Wilaya ya Rufiji kuchangamkia fursa za kutoa huduma kwa wafanyakazi wanaojenga mradi wa umeme wa maji wa Mto Rufiji.


“Vijana nendeni Ngarambe, Mloka na Mwasemi, ajira ziko za kutosha, akina mama ntilie, wanatakiwa vibarua, lakini pia kunachangamoto ya nyumba za kulala wageni, kwa hivyo ziko fursa nyingi katika maeneo ya mradi.” Alisema.


Alisema kuna mahitaji mbalimbali ya vyakula kama vile mbogamboga, kitoweo, mahitaji ya bidhaa hizo yamekuwa makubwa na kutoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Rufiji kuhcngamkia fursa hiyo.