Bomu lililokuwa linasafirishwa kutoka Serengeti kwenda Mkoa wa Mwanza kuuzwa kama vyuma chakavu limegundulika katika gari la mfanyabiashara wa vyuma chakavu.

Mfanyabiashara huyo mkazi wa Mugumu Serengeti mkoani Mara, Jonas Marwa anasema wakati anapakia mzigo kwenye gari ndipo alipogundua kuwa kuna chuma ambacho sicho cha kawaida kwenye mzigo huo.

Naye Mkuu wa Polisi wilaya ya Serengeti, Methiew Mgema anasema kuwa mara baada ya kuona chuma kisicho cha kawaida, mfanyabiashara huyo alienda kutoa taarifa kituoni na ndipo wakaenda kukagua na kukabaini kuwa ni bomu.

Mara baada ya kuliteketeza bomu ilo na maafisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kikosi cha 27, Afisa wa Kikosi hicho, Meja Patrick Kitosi ametoa wito kwa wafanyabiashara wa vyuma chakavu na wananchi wote kutoa taarifa pindi wanapoona vyuma ambavyo siyo vya kawaida.