MSANII wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka na mwanamuziki wa Kizazi Kipya aliyekuwa akimsimamia kazi zake Said Kassim a.k.a Casso wamemwagana rasmi baada ya kutofautiana kimaslahi.Akizungumza na Za Motomoto, Casso anayetamba na ngoma mbalimbali ikiwemo Kitonga alisema ameamua kuachana na Rose baada ya kushindwa kuafikiana makubaliano waliyowekeana.Kuna mambo mengi tulikuwa tumekubaliana lakini yakawa yanaenda ndivyo sivyo ndipo nikaamua kutafuta kampuni nyingine ya Haffiyy Entertainment ambayo nafikiri tunaweza kwenda sambamba.

“Unajua muziki ndiyo maisha yangu sasa nilipoona mambo yanakwenda ndivyo sivyo nikaona nichukue uamuzi mapema.” Alisema Casso.Rose alipoulizwa na Za Motomoto kuhusiana na kutemana na msanii huyo alisema; “Kuondoka kwake kwangu hakuna kilichopungua kama anatafuta maisha basi mimi namtakia maisha mema ila suala la kutomtimizia tuliyokubaliana tatizo lake ilikuwa ni uhitaji wa haraka wakati mambo mazuri hayataki haraka.” Alimaliza kusema Rose.