Wanafunzi wakionyesha jumbe za mabango kwenye ufunguzi wa michezo ya (UMISSETA) Mkoani Shinyanga.

Awali mgeni Rasmi mkuu wa mkoa wa Shinyanga akiwasili kwenye uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga Mjini kwa ajili ya kufungua michezo hiyo ya shule za sekondari UMISSETA.

Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack katikati akiwasili kwenye uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga Mjini kwa ajili ya kufungua michezo hiyo ya UMISSETA.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akizungumza kwenye ufunguzi wa michezo ya UMISSETA kwa shule za Sekondari mkoani Shinyangana kuwataka wanafunzi waitumie michezo hiyo kuonyesha vipaji vyao, ikiwa michezo ni afya pamoja na ajira na kukemea shule binafsi ambazo zimezuia wanafunzi wao wasishiriki michezo hiyo.

Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga Mohamed Kahundi akisoma risala kwenye ufunguzi wa michezo hiyo ya UMISSETA na kumuomba mgeni rasmi mkuu wa mkoa kuwatafutia wafadhili ambao watakuwa wakifadhili michezo hiyo kila mwaka pamoja na halmashauri kutenga fedha za mapato ya ndani, ili kuondoa changamoto ya ukata wa Fedha na kusababisha kufanya vibaya kwenye mashindo ya kitaifa kama ilivyotokea mwaka jana.

Awali mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akimkaribisha mkuu wa mkoa huo wa Shinyanga Zainab Telack kufungua michezo hiyo ya UMISSETA kwa shule za sekondari ambayo itadumu kwa muda wa siku tatu.

Wanafunzi wakiwa kwenye ufunguzi wa mashindano ya michezo ya UMISSETA Mwaka (2019) mkoani Shinyanga yaliyofanyika kwenye uwanja wa michezo wa CCM Kambarage.

Wanafunzi wakiwa kwenye ufunguzi wa michezo ya (UMISSETA) Mkoani Shinyanga.

Wanafunzi wakiwa kwenye ufunguzi wa michezo ya (UMISSETA) Mkoani Shinyanga.

Awali wanafunzi wakiingia kwa maandamano kwenye ufunguzi wa michezo hiyo ya Shule za Sekondari (UMISSETA) Mkoani Shinyanga.

Wanafunzi wakiingia kwa maandamano kwenye ufunguzi huo wa michezo ya UMMISETA.

Wanafunzi wakiimba nyimbo ya taifa kwa ajili ya kuwa tayari kufungua michezo hiyo ya shule za Sekondari (UMISSETA) Mkoani Shinyanga. Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.

Mashindano ya Umoja wa Michezo na Sanaa kwa shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA 2019) yamefunguliwa rasmi mkoani Shinyanga, ambapo wanafunzi wataonyesha vipaji vyao kwa kushiriki katika michezo mbalimbali.Mashindano ya (UMISSETA 2019) yamefunguliwa leo Mei 27,2019 na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainabu Telack kwenye viwanja vya michezo vya CCM Kambarage Shinyanga Mjini na kuhudhuriwa na wanafunzi wa shule za sekondari kutoka halmashauri sita za mkoa huo sambamba na kusindikizwa na wadogo zao wa shule za msingi.

Michezo ambayo itashindaniwa ni mpira wa miguu, mpira wa pete, kikapu, wavu, riadha, mpira wa meza, kucheza ngoma, pamoja na kuimba kwaya, ambayo itadumu kwa muda wa siku tatu, ambapo washindi watakwenda kushindana kitaifa.

Akifungua mashindano hayo,Telack aliwataka wanafunzi hao kudumisha nidhamu kwenye mashindano hayo hata wale ambao watachaguliwa kwenda Mtwara kushiriki kitaifa wakaonyeshe nidhamu ya hali ya juu.

Alisema michezo ni afya, humjenga mtoto kiakili,kinidhamu, kuibua vipaji na hivyo kusikitishwa na shule binafsi ambazo zimezuia wanafunzi wao kushiriki kwenye michezo hiyo na kuwataka waiche tabia hiyo mara moja, ikiwa huko ni kumnyima mtoto kuonyesha kipaji chake na kuweza kupata ajira hapo baadae.


“Kuna taarifa tunazo eti baadhi ya shule binafsi zimezuia wanafunzi wao kutoshiriki michezo hii ya UMISSETA, ni jambo la ajabu sana, mfano baba yake na Mbwana Samatta angekuwa wakimzuai mtoto wake kushiriki kwenye michezo leo asingekuwa mchezaji wa kimataifa, hebu waruhusuni watoto wenu  waonyeshe vipaji vyao kwani michezo ni ajira pia,”aLIsema Telack.

“Na niye wanafunzi ambao mnashiriki michezo hii ya UMMISSETA naombeni muonyeshe vipaji vyenu ambavyo mmepewa na Mungu, pamoja na kudumisha nidhamu ya hali ya juu hata huko mtakapokwenda Mtwara na siyo kwenda kuendekeza mapenzi, nataka muje na makombe hapa ya ushindi likiwEmo la nidhamu,”aliongeza.

Pia aliziagiza halmshauri zote za mkoani humo kutenga bajeti ya kila mwaka wa fedha shilingi Milioni 2 kwa ajili ya kufanikisha michezo hiyo ya UMISSETA licha ya kupata fedha zingine kutoka wahisani ili kuwa rahisishia maisha wanafunzi wakaokuwa kambini.

Kwa upande wake Afisa Elimu mkoa Shinyanga Mohamed Kahundi akisoma risala ya ufunguzi wa michezo hiyo ya UMMISSETA, alisema changamo ambayo wanakabiliana nayo kuendesha mashindano hayo hadi ngazi ya taifa ni ukata wa fedha na hivyo kuomba wahisani waendelee kujitokeza kufadhili michezo hiyo.

Alisema kwa mwaka jana (2018) mkoa ulifanikiwa kupeleka timu kwenye mashindano ya kitaifa, lakini haukufanya vizuri kwani ulishika nafasi ya 20 kati ya 28 sababu ya maandalizi kuwa mabaya kutokana na upungufu wa rasilimali fedha ambapo hata baadhi ya timu zilishindwa kuzipeleka kushiriki kwenye mashindano hayo.

Kauli mbiu ya  (UMISSETA) mwaka huu inasema "michezo na sanaa kwa elimu bora na ajira".