Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda ametoa shukrani kwa wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa upendo mkubwa waliomuonyesha.

RC Makonda amesema kuwa ila anaondoka akiwa na maumivu makubwa kwani amemuacha rafiki na baba yake katika ardhi.

"Asanteni sana ndg zangu wa Kilimanjaro Kwa upendo mkubwa mlionionyesha. Naondoka bado nikiwa namaumivu makubwa sana kwani nimemwacha rafiki na Baba katika Ardhi siyo kama nilivyozoea," ameandika Makonda katika ukurasa wake wa mtandao wa Kijamii.