Mwanamuziki wa Bongo Fleva kutoka WCB, Rayvanny, amewafanyia jambo la kushangaza madereva bodaboda na bajaji ambao wamebandika stika za picha yake na kuchora jina lake kwenye vyombo vyao hivyo vya moto.Rayvanny amewapiga tafu madereva hao katika maeneo ya Sinza Mori jijini Dar es Salaam na kusema miongoni mwa watu ambao wamekuwa wakisapoti kazi zake kwa muda mrefu ni pamoja na madereva wa bodaboda na bajaji hivyo kwa kutambua mchango wao ameamua kurudisha shukrani kwa staili hiyo.Rayvanny anatarajia kufanya bonge moja la shoo Sikukuu ya Eid Pili katika Uwanja wa Taifa wa Burudani DAR LIVE Uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar.