RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar, katika mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara hiyo iliofanyika Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar, kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na kulia Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe.Dkt. Sira Ubwa.
BAADHI ya Maofisa wa Idara za Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji wakifuatilia mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.
WAZIRI wa Ujenzi Mawasiliani na Usafirishaji Zanzibar Mhe.Dr. Sira Ubwa akiwasilisha Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara yake wakati wa mkutano huo uliofanyika Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar, ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein
BAADHI ya Maofisa wa Idara za Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji wakifuatilia mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.
KATIBU Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Ndg. Mustafa Aboud Jumbe akiwasilisha Vifungu vya Matumizi na Mapato ya Wizara yake wakati wa Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai 2018 hadi March 2019, katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.(Picha na Ikulu)