Rais wa Marekani, Donald Trump amesema nchi yake haiko tayari kufikia makubaliano ya kibiashara na China, lakini anaacha wazi uwezekano wa mataifa hayo mawili siku moja kufikia makubaliano.

Akizungumza jana mjini Tokyo, Trump amesema China iko tayari kufikia makubaliano, lakini Marekani haiko tayari.

Mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa duniani yamekuwa katika mzozo wa kibiashara. Trump anatarajiwa kukutana na Rais wa China, Xi Jinping mwezi ujao katika mkutano wa mataifa yenye nguvu kiuchumi, G20.

Aidha, Trump pia amekutana na Mfalme Naruhito wa Japan katika kasri la kifalme. Mfalme huyo pamoja na mkewe Masako wamemkaribisha Trump, kiongozi wa kwanza wa kigeni tangu Naruhito alipotawazwa hivi karibuni. Trump amekutana pia na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe.