Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali mbele ya Makaburi ya Mashujaa wa Namibia yaliyopo katika eneo la Heroes’ Acre mara baada ya kuweka shada la maua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kuweka shada la maua katika Makaburi ya Mashujaa wa Namibia yaliyopo katika eneo la Heroes’ Acre mara baada ya kuwasili katika eneo hilo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka pamoja na mwenyeji wake Rais wa Namibia Hage Geingob mara baada ya kuweka shada la maua katika Makaburi ya Mashujaa wa Namibia yaliyopo katika eneo la Heroes’ Acre
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mwenyeji wake Rais wa Namibia Hage Geingob mara baada ya kuweka shada la maua katika Makaburi ya Mashujaa wa Namibia yaliyopo katika eneo la Heroes’ Acre.
---
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Mei, 2019 ametembelea na kuweka shada la maua katika eneo la mashujaa (Heros Acre) waliopigania ukombozi wa Namibia, lililopo nje kidogo ya Jiji la Windhoek nchini humo. 

Katika eneo hilo wamezikwa mashujaa wa ukombozi wa Namibia ambao baadhi yao walipata mafunzo katika kambi ya Kongwa nchini Tanzania, wengine walikuwa maafisa wa Chama cha SWAPO ambao ofisi zao zilikuwa Jijini Dar es Salaam na wengine ni viongozi wakuu walioendesha mapambano wakiwa nchini Namibia. 

Baadhi ya mashujaa waliozikwa katika eneo hilo ni Ndimo Hamaambo, Peter Nanyemba, Theo-Ben Gurirabo na Toiro ya Toire. 

Mhe. Rais Magufuli ameongozana na mwenyeji wake Mhe. Rais Hage Geingob.