Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Magufuli amempandisha hadhi aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Juma Homera kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi kuanzia leo, Mei 14,2019.

Uteuzi huo wa Homera umetokana na uamuzi wa wa Rais kumpumzisha aliyekuwa mkuu wa mkoa huo, Amos Makala na kwamba uteuzi wa mkuu wa Wilaya ya Tunduru utafanywa baadaye.

Homera aliteuliwa kuiongoza Wilaya ya Tunduru mwaka 2016 na mpaka anapandishwa wadhfa huu, alikuwa hajahamishwa eneo hilo la kazi.

Kabla ya kupelekwa Katavi Julai mwaka jana, Makalla alikuwa mkuu wa Mkoa wa Mbeya alikodumu tangu mwaka 2016 Dkt. Magufuli alipofanya uteuzi wa kwanza wa wakuu wa mikoa na wilaya.