RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuika na Wafanyakani wa Benki ya Watu wa Zanzibar na Wananchi katika futari ilioandaliwa na PBZ, katika hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar jana 20-5-2019.(Picha na Ikulu)
 WAZIRI wa Biashara na Viwanda Zanzibar kushoto Mhe. Balozi Amina Salum Ali, akiwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Bi. Khadija Shamte, wakipata futali ilioandaliwa na PBZ kwa Wateja wao na Wananchi iliofanyika katika ukumbii wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar jana 20-5-2019.
 MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar Bi. Kidawa Himid. Saleh, akijumuika na Wananchi katika Futari maalum ilioandaliwa na PBZ katika hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.
 WAGENI waalikwa wakipata futari katika hoteli ya Verd Mtoni Zanzibar ilioandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd.(PBZ)
 .
 WANANCHI wa Zanzibar wakijumuika na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, katika Futari ilioandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) katika Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi mbalimbali meza kuu kushoto Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Balozi Mohamed Ramia, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na kulia Mjumbe wa Bodi ya PBZ Yakout Hassan Yakout , Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, wakimsikiliza Sheikh Abdalla Talib akitowa nasaha baada ya kumalizika hafla hiyo ya futari katika ukumbi wa hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar
 MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akitowa neno la shukrani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa hafla hiyo ya futari ilioandaliwa na PBZ katika hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiitikia dua ikisomwa na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Othman Hassan Ngwali, baada ya kumalizika hafla ya futari ilioandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar katika Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na kuagana na Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg. Juma Ameir Hafidh baada ya kumalizika kwa hafla ya Futari iliofanyika katika Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar katikati Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Balozi Mohammed Ramia Abdulwawa.(Picha na Ikulu)